SoC04 - Nini kifanyike kuboresha utendaji wa wawakilishi ili kuleta Demokrasia yenye tija kwa Maendeleo ya Taifa (2024)

UTANGULIZI
Demokrasia ya kweli ni uwezo mkubwa wa taifa katika uwasilishaji wa mawazo utakao ruhusu kupokea mitazamo kwa kila mwananchi. Katika kuzingatia hilo uwakilishi wa maamuzi kitaifa hufanywa na watu wachache wanao chaguliwa na wananchi wote. Umuhimu wa wakilishi upo kwenye kila nyanja ya maendeleo kuanzia kiuchumi, kielimu, kidemokrasia, haki pamoja na utawala bora. Bunge ni muhimili unaoundwa na wawakilishi waliopewa dhamana kitaifa katika utungaji wa sheria ili kusimamia rasilimali na maendeleo kiujumla.

Uboreshwaji wa utendaji wa wakilishi unabeba tija kubwa kwa maendeleo ya taifa katika nyanja zote kitaifa. Wananchi wote tunategemea wawakilishi kama wasimamizi wetu kwenye matumizi ya rasilimali za umma ambao unasimamiwa na serikali kuu. Maana halisi ya uwakilishi ni kwamba endapo wataridhia jambo ni wananchi wote wameridhia na endapo watakataa jambo ni wananchi wote wamekataa. Kwa dhana hii tunaitaji mawazo ya wananchi ni kwanamna gani wawakilishi watatenda kazi kiuhakika.
Kufikia tanzania tuitakayo yenye wawakilishi wanao wakilisha wawazo ya wananchi nashauri haya yafanyike

1. Wawakikilishi wasitokane na chama kilicho shikilia madaraka.
Inashangaza kuona badala ya wawakilishi kuwakilisha wananchi kwa serikali wanakua wawakilishi wa serikali kwa wananchi. Hii inatokana na hali ya uongozi wa chama ulichoshika serikali kua uongozi wa chama cha wawakilishi. Napendekeza kupata wawakilishi wasiokua na chama kilicho unda serikali yani tue na mfumo wa vyama vya aina mbili vyama vya mfumo wa uwakilishi na vyama vya mfumo wa kiserikali

Kuruhusu wawakilishi wa kujitegemea, hawa ni wawakilishi wasio fungamana na upande wowote hii itapelekea wao kusimamia kile ambacho wananchi wao wamewatuma wakawawakilishe. Lakini ukitoa wawakilishi wa mahali kuwe na wawakilishi kitaasisi mfano mwakilishi wa kilimo, mwakilishi wa elimu mwakilishi wa utalii nao wawepo katika mamlaka za uwakilishi.

2. Matumizi ya teknolojia katika maamuzi kwa wawakilishi.
Niwazi kua mfumo ambao wawakilishi wetu hutumia kuafikiana umepitwa na wakati, mfumo wa kuitikia ndio kwa pamoja bado auna usiri kwenye kura. Kutokana na maboresho ya teknolojia kunaweza kuwa na vitufe vya ndio na hapana vitakavyo saidia kupata maamuzi sahihi ya maridhiano kwa usiri mkubwa.

3. Mfumo wa kidijitali wa kuwasilisha mawazo ya wananchi kwa wawakilishi wao.
Japo kua wawakilishi wanawakilisha wananchi ila amna namna ambayo wawakilishi hawa hupata mawazo kwa watu wao. Napendekeza mfumo uwekwe ambao wananchi wote watashiriki kwenye jukwaa katika kutoa mawazo yao, hii ni kwasababu ukuaji wa kidijitali unafikia watu wengi badala ya kulalamika kwenye mitandao ya kijamii basi uo mfumo ukutanishe wananchi na wawakilishi wao.

4. Sheria ya kusitisha uwakilishi kabla ya muhula kuisha.
Wananchi ndo wenye dhamana ya kuchagu wawakilishi wanao wataka kikatiba, lakini wananchi hao hawana dhamana ya kumtoa kwenye uwakilishi endapo itaonekana kushindwa. Napendekeza wawakilishi wasiwe na dhamana ya kudumu, pale ambapo itaonekana hawawakilishi ipasavyo apokonywe mamlaka na kupewa mtu mwengine.

5. Kuanzishwa kwa chombo muhimu cha kuwaadhibu wabadhilifu wanao bainishwa na CAG.
Japo kuna muhimili unaosimamia sheria lakini wawakilishi wapewe mamlaka yakuanzishwa kwa kitengo au kamati ya ufuatiliaji wa ripoti ya mkaguzi wa serikali. Kitengo hichi kitafuatilia ripoti baada ya kujadiliwa na kila atakae bainika kuhojiwa na wawakilishi na kupelekwa kamati ya ubadhilifu kisha kupewa adhabu stahiki. Napendekeza kuwe na sheria itakayo ruhusu wabadhilifu kutangazwa pamoja na adhabu zao ili kue na funzo kwa viongozi wote.

6. Kazi ya uwakilishi kuwa ya kitaalamu.
Katiba inaruhusu mtu yeyote mwenye sifa kuweza kuomba kuwa mwakilishi na kupata ridhaa ya wananchi, lakini sasa napendekeza kuwe na wawakilishi wenye weledi na ambao wana elimu ya uongozi na wawe wamepita ngazi mbali mbali za uongozi na kupimika kimaendeleo mfano mwakilishi kitaifa aanze kua mwakilishi mtaa kisha kata ndo awe mwakilishi wa jimbo. Watu wengi wanaona uongozi ni kama fursa sehemu ambayo utakaa kaa tu unapata mshahara na posho alafu unatajirika. Kuondoa hii dhana mwakilishi anapaswa kupimwa kwa utimizi wa ahadi kwenye maisha ya uongozi ngazi za chini.

Ili kuipa mkazo taaluma ya uongozi ilinganishe na taaluma nyingine kiweledi. Hii itafanya baadhi ya taluma za uzalishaji kuonekana bora zaidi kuliko taaluma ya uongozi.

7. Ratiba ya kitaifa ya wawakilishi kuonana na wananchi wao.
Inasikitisha kusikia wananchi wakisema baadhi ya viongozi wakisha chaguliwa kuonekana ni mpaka uchaguzi ujao. Kama ilivyo ada kua na ratiba ambayo wawakilishi hukutana kitaifa basi mamlaka zinazosimamia wawakilishi ziwe na ratiba pia ambazo zitawalazimu wawakilishi wakaonane na wananchi wao. Hii itasaidia kuwafikia wananchi wengi na kupokea mawazo yao kwa pamoja.

HITIMISHO
Kwa ujumla kuona wawakilishi ambao wanawakilisha mawazo ya wananchi ni hatua kubwa katika maendeleao ya demokrasia nchini. Kila mwananchi anatamani kuona mawazo ya walio wengi katika majimbo yanatumika ngazi ya maamuzi. Natoa rai kwa wawakilishi kuweza kutenga muda wa kuonana na wapiga kura wao kwa ratiba husika ili kukusanya kero zao. Si vyema kuona mwakilishi akikosoa hoja na mwishowe kuiunga mkono. Wawakilishi wafanye kazi za wanao wawakilisha.

SoC04 - Nini kifanyike kuboresha utendaji wa wawakilishi ili kuleta Demokrasia yenye tija kwa Maendeleo ya Taifa (2024)

References

Top Articles
Latest Posts
Article information

Author: Domingo Moore

Last Updated:

Views: 6069

Rating: 4.2 / 5 (53 voted)

Reviews: 84% of readers found this page helpful

Author information

Name: Domingo Moore

Birthday: 1997-05-20

Address: 6485 Kohler Route, Antonioton, VT 77375-0299

Phone: +3213869077934

Job: Sales Analyst

Hobby: Kayaking, Roller skating, Cabaret, Rugby, Homebrewing, Creative writing, amateur radio

Introduction: My name is Domingo Moore, I am a attractive, gorgeous, funny, jolly, spotless, nice, fantastic person who loves writing and wants to share my knowledge and understanding with you.